Darasa ni la Digital Electronics na sielewi analolifunza mwalimu.Usitake* jua wivu ninao kwa wanagenzi wenzangu wanaolielewa somo hili ninavyoelewa kula. Sijui kama ni kwa sababu sina raha na cheti ninachokitafuta hapa, kawaida yangu ama ni siku tu isiyo njema kwangu. Hilo halihusishi sana. Nilipokuwa nimezubaa wazo likanijia la kuandika nukuu hii kwa Kiswahili. Sio kawaida, hata ninavyohisi ni kama wazimu wa aina fulani. Nilitumia Kiswahili andishi miaka kama saba hivi iliyopita. Mimi ni mojawapo ya wale ambao Kiswahili hutatiza wakati ufikapo wa kukiandika na kujieleza. Matumizi ya lugha pia nashuku nimekiuka sheria kadha nabado nitaendelea kizikiuka niendeleapo na makala haya. Siwezi andika ng’ano ya maana sana vile nikitumia hii lugha kwa sababu, wengi hawataelewa, lakini kwa sababu fikra hiyo imenipata, lazima ningejipa motisha na niandike kwa lugha ya Kiswahili.
Pale mwanzo sijui nilitoa wapi hilo wazo la kutumia lugha hii,lakini nimekumbuka sasa…. Leo nimekuwa tu nimejipoteza kwa mawazo, na nikafikiri kunukuu mawazo hayo kwa mtandao nikipitia Facebook na Twitter. “Huu ndio mwezi ulioanza kama nimeinua mkono na kulingana na maono, utaisha nikiwa hivo hivo – Julai”. Wazo lingine likafuata kuwa,watakaosoma watabaki wameshangazwa na tamko hilo (Kawaida yao) Nilitupilia wazo hilo mbali na mahali lilipoanguka, wazo la kuandika nukuu kwa lugha ya Kiswahili likanipata. (Samahani lakini, kila wakati najipata nimeandika ‘Kishwahili’)

Hapo awali nilijaribu kueleza ugumu wa kujieleza kwa Kiswahili. Wengi huwa hawapendi kuisoma lugha hii na ndio kwa sababu nitakoma kuandika makala haya hivi karibuni. Lakini wasomaji wakipenda nitaendelea tu. Hakuna namna (‘Kijeshi’)
Nikimalizia, nimeamua kujipa motisha wa kuandika ili niwe na nidhamu ya kumaliza ninayoyaanza. Hii ni mojawapo ya malengo ambayo nimeyanukuu kutekeleza mwaka huu. Kwenye orodha ya makala yanayongoja kuendelezwa ni Visa vya Liam, How I Joined The Military, na Career Path.
Endelea kuburudika Msomaji mpendwa.
Endelea kuburudika Msomaji mpendwa.
Kiswahili Kitukuzwe!!!
Cool!